Mshambuliaji
wa kimataifa wa Togo Emmanuel Adebayor, miezi ya hivi karibuni amekuwa
na akipitia kipindi kigumu katika klabu yake ya Tottenham Hotspur, huku
pia akisakamwa na matatizo ya kifamilia kiasi cha kufikia hatua ya
kuandika katika ukurasa wake wa Facebook .
Mwezi Mei mwaka huu, Tottenham walimpa muda wa mapumziko ili aweze kupata wasaa wa kusuluhisha matatizo yake ya kifamilia.
Huku
mustakali wake na klabu yake ukiwa bado haujulikani, mshambuliaji huyo
wa zamani wa Arsenal na Manchester City, leo ameamua kusilimu na kuwa
Muislamu.
Katika
video hapo chini Emmanuel Adebayor, Adebayor anaonekana akitoa shahada
(akishahadia, ishara ya Kiislamu inayoashiria kumkubali Mungu na
Muhammad kuwa ndiye Mtume wake), na kuthibitisha kuwa sasa amekuwa
Muislamu rasmi.

0 comments:
Post a Comment