عَنْ
ابْن مَسْعُودٍ (رضي الله عنه) أنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ
عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَال: ((إِذَا كُنْتُمْ ثلاَثَةً فلاَ يَتَنَاجَى
اثْنَانِ دُونَ الآخَرِ حَتَّى تَخْتَلِطُوا بِالنَّاسِ مِنْ أَجْلِ أَنْ
يُحْزِنَهُ)) متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) kwamba Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Mnapokuwa
watatu, basi wawili wasinong’onezane bila kumshirikisha mwengine hadi
wajiunge watu wengine [kumtoa katika upweke yule aliyeachwa katika
mazungumzo] na watu, kwa sababu kufanya hivyo kutamhuzunisha [yule wa
tatu])).[1]
Mafunzo Na Hidaaya:
- Makatazo ya kunong’onezana wawili anapokuweko mtu wa tatu ili asiudhike na kuhisi vibaya.
- Kunong’onezana mbele ya wengineo huenda kukasababisha kutia shaka au dhana mbaya kwa ambaye hakushirikishwa katika mnong’ono.
- Makatazo ya kunong’onezana pasi na kuwashirikisha wengineo hata ikiwa ni zaidi ya idadi iliyotajwa na hata kwa jambo la kheri haipasi. Na kwa jambo la shari Amekataza Allaah (سبحانه وتعالى). [Al-Maaidah 5: 2].
يَا
أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا تَنَاجَيْتُمْ فَلَا تَتَنَاجَوْا
بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَمَعْصِيَتِ الرَّسُولِ وَتَنَاجَوْا
بِالْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٩﴾ إِنَّمَا النَّجْوَىٰ مِنَ الشَّيْطَانِ لِيَحْزُنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَلَيْسَ بِضَارِّهِمْ شَيْئًا إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١٠﴾
Enyi
mlioamini! Mnaponong’onezana, basi msinong’onezane kwa (mambo
yanayohusu) dhambi na uadui na kumuasi Mtume (lakini) nong’onezaneni kwa
(mambo yanayohusu) wema na taqwa; na mcheni Allaah Ambaye Kwake Pekee
mtakusanywa (nyote). Hakika mnong’ono ni kutoka kwa shaytwaan ili
awahuzunishe wale walioamini, na wala hawezi kuwadhuru chochote
isipokuwa kwa idhini ya Allaah. Na kwa Allaah (Pekee) watawakali
Waumini.[2]
- Uislamu unapendelea amani baina ya ndugu na kufunza adabu njema na njia za kuepusha kila aina ya maudhi au maovu ya nafsi.
- Kutokunong’onezana ni katika adabu za kikao baina ya Waislamu.
- Athari ya hivyo ni mbaya, kwani dhana hiyo mbaya inaweza kuzaa uadui na chuki.
0 comments:
Post a Comment