KUNDI la wanamgambo wa Islamic State limewaua mateka takribani 300 ambao ni raia wa Yazidi kaskazini mwa Iraq.
Makamu wa rais nchini Iraq, Osama al-Nujifi ameyalaani mauaji hayo akiyataja kuwa ya kikatili.
Taarifa zimeeleza kuwa watu hao waliuawa katika wilaya moja iliyo magharibi mwa mji wa Mosul siku ya Ijumaa.
Wanamgambo wa Islamic State walithibiti maeneo yaliyo kaskazini mwa
Iraq kwa karibu mwaka mmoja uliopita ambapo waliwaua na kuwashika mateka
maelfu ya watu wa Yazidi wakiwaita makafiri.
Chanzo: BBC
- Blogger Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment