Akiwahutubia waumini walioshiriki maandamani hayo, Imam wa msikiti huo, Hemed Jalala, amewataka waumini wa Kiislamu na wasio waislamu kudumisha amani ili kuepuka machafuko.
“Viongozi wa dini tuhimize waamini wetu katika kuliombea amani taifa letu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, Mungu ambariki kiongozi anayemaliza kipindi chake lakini pia atuongoze katika kumchagua kiongozi mwingine aliyekuwa bora na mwenye kupenda amani ili kuliepusha taifa na machafuko kama yanayozikumba nchi zingine za Kiarabuni ikiwemo Palestina,’’ alisema Jalala.
0 comments:
Post a Comment