Dr. Othman, alivitaja aina ya vyakula hivyo kwa ajili ya futari kwa Waislamu hao kuwa ni Mchele, Sukari, Unga wa Ngano, Mafuta ya kupikia, Maharage, pamoja na Tende.
Mkurugenzi huyo aliitaja Mikoa mingine iliyobahatika kupata futar hiyo kuwa ni Iringa, Tanga, Moshi pamoja na Bukoba, ambapo jumla ya Shilingi Milioni mia mbili, zimetumika katika kuwafuturisha Waislam hao.
Dr. Othman, ametoa wito kwa Waislamu wenye uwezo na Taasisi mbali mbali kujenga tabia ya kuwasaidia masikini na wale wasio na uwezo wa kumudu kupata futari kwani akasema, kufanya hivyo ni katika kutekeleza maamrisho ya Allah (s.w) katika Uislamu na ni sawa na kukujiwekea akiba ya akhera yao.
Aidha, Mkurugenzi huyo amewanasihi Waislamu kujitahidi kufanya ibada mbali mbali katika mfungo huu Mtukufu wa Ramadhani kwa lengo la kupata fadhila za Allah (S.W).
Africa Muslim agency ni Taasisi ya kidini inayoshughulika na mambo mbalimbali yanayohusu Waislamu, kama vile kuchimba visima vya maji, kujenga Misikiti pamoja na kuendesha Shule.
0 comments:
Post a Comment