24-Wanyama Na Alivyoumba Allaah Vinathibitisha Tawhiyd

Hud-hud (ndege) alikuwa miongoni mwa jeshi la Nabiy Sulaymaan (‘Alayhis-Salaam). Aliporuka na kufikia mji wa Sabaa alikuta watu huko wanaabudu jua, akarudi kumpa taarifa Nabiy Sulaymaan (‘Alayhis-Salaam) kwa kuikansuha ‘ibaadah hiyo batili. Uzuri ulioje ndege huyo kuthibitisha Tawhiyd ya  Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa)! Kisa chake kinaanza katika Qur-aan pale alipokosekana katika jeshi la Nabiy Sulaymaan (‘Alayhis-Salaam):
وَتَفَقَّدَ الطَّيْرَ فَقَالَ مَا لِيَ لَا أَرَى الْهُدْهُدَ أَمْ كَانَ مِنَ الْغَائِبِينَ ﴿٢٠﴾ لَأُعَذِّبَنَّهُ عَذَابًا شَدِيدًا أَوْ لَأَذْبَحَنَّهُ أَوْ لَيَأْتِيَنِّي بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ ﴿٢١﴾ فَمَكَثَ غَيْرَ بَعِيدٍ فَقَالَ أَحَطتُ بِمَا لَمْ تُحِطْ بِهِ وَجِئْتُكَ مِن سَبَإٍ بِنَبَإٍ يَقِينٍ ﴿٢٢﴾ إِنِّي وَجَدتُّ امْرَأَةً تَمْلِكُهُمْ وَأُوتِيَتْ مِن كُلِّ شَيْءٍ وَلَهَا عَرْشٌ عَظِيمٌ ﴿٢٣﴾ وَجَدتُّهَا وَقَوْمَهَا يَسْجُدُونَ لِلشَّمْسِ مِن دُونِ اللَّـهِ وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ فَصَدَّهُمْ عَنِ السَّبِيلِ فَهُمْ لَا يَهْتَدُونَ ﴿٢٤﴾ أَلَّا يَسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِي يُخْرِجُ الْخَبْءَ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَيَعْلَمُ مَا تُخْفُونَ وَمَا تُعْلِنُونَ ﴿٢٥﴾ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ ۩﴿٢٦﴾
(Sulaymaan) Akakagua ndege, akasema: “Imekuwaje, mbona simuoni Al-Hud-hud, au amekuwa miongoni mwa walioghibu? Bila shaka nitamuadhibu adhabu kali, au nitamchinja, au aniletee hoja bayana (ya kughibu kwake).” Basi hakukaa sana (mara alitokeza) akasema: “Nimegundua usilogundua na nimekujia kutoka Sabaa na habari za yakini. Hakika mimi nimemkuta mwanamke anawamiliki, na amepewa kila kitu, na anacho kiti cha enzi kikubwa. Nimemkuta (yeye) na watu wake wanalisujudia jua badala ya Allaah, na shaytwaan amewapambia ‘amali yao (hiyo), basi akawazuia na njia (ya haki); kwa hiyo hawakuongoka. Hawamsujudii Allaah Ambaye Anatoa yenye kufichika katika mbingu na ardhi na Anayajua yale mnayoyaficha na yale mnayoyadhihirisha. Allaah - hakuna ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye, Rabb (Mola) wa Al-‘Arsh adhimu. [An-Naml: 20-26]
Share on Google Plus

About mfaume

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment